Jumanne, 29 Julai 2025

Maneno ya kiswahili na kigerenza

English👉Swahili

Yawn 👉Miayo
Snore 👉Kukoroma
Sneeze👉Chafya
Hiccup👉Kwikwi
Cough👉Kikohozi
Folding 👉Kukuja nguo
Crumple👉Kukuja karatasi
Break👉Kuvunja
Shake👉Kutikisa 
Press👉Bonyeza
Drop👉Shusha
Changer 👉Imekamilika yote
Cable👉yuesibi
Plug👉Kichwa cha chanja

Jumamosi, 26 Julai 2025

NDOTO ZA MAGARI

NDOTO ZA KUOTA MAGARI. 

Zekaria 6:1
Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba.

Auburn:33:14-15.
NDOTO ni Taarifa Ya Jambo linalokuja au liliopo au lilishapita
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa LA Holy Spirit church Tanzania

NDOTO za Kuota MAGARI humani Mambo yafatayo Kwenye Ulimwengu wa roho.

1:Gari au Usafiri humanisha Baraka za kimwili na rohoni. 

2:Humanisha Huduma au Kazi Mtu Anayokuwa Anaifanya. 


NDOTO NA TAFSIRI SAKE. 

1:Ukiota upo sted gari limekuacha👉 Unajulishwa Maendeleo uliyonayo yatacheleweshwa kiroho na kimwili. 
Omba kukataa Kucheleweshwa

2:Ukiota Unaendesha gari👉Unajulishwa Huduma au Kazi Yako itaenda Vizuri mno.
Omba bariki NDOTO hii
3:Ukiota Umeharibikiwa Gari👉Unajulishwa Kazi Yako inaenda kuingia shida ya kuyumba. 
Omba Kukataa ndoto hii. Nakataa kuhabika kwa Kazi kwa Jina LA Yesu. Ameen

4:Ukiota Upo Kwenye rami MAGARI yanakuja mengi uliposimama👉Unajulishwa Kuna Baraka Zitafuguka kwako. 
Ombea Hii NDOTO Kusema Mungu Timiza ndoto hii. 

5:Ukiota Unaendesha Gari Kwenye Milima👉Unajulishwa Maendeleo ya Kazi Yako itapita Kwenye misukosuko. 
Omba Kukataa ndoto hii. 

6:Ukiota Gari limepaki sted nawewe umekaa Kwenye Gari haliendi👉Unajulishwa Huduma au Kazi Zako Zitasimama hazitaendelea Vizuri Kama Mwanzo. 
Omba hii taarifa kataa.

7:Ukiota Unajifunza Kuendesha Gari👉Unajulishwa Unapaswa ujifunze kufanya huduma uliyonayo. 
Tafuta wachungaji wakusaindie kukuombea. 

8:Ukiota Upo Kwenye Gari LA Rais👉Unajulishwa Unaenda Kufanya Kazi na Viongozi wakubwa. 
Ibariki ndoto hii ukiota Mwambie Bwana iwe kweli. . 

9:Ukiota Gari Kubwa👉Unajulishwa Una huduma  Kubwa Sana ndani Yako. 

10:Ukiota Gari ndogo👉Unajulishwa huduma ndogo uliyonayo

Unatakiwa ichochee nakuiombea

11:Ukiota Magari ya Vita Yanakuja uliposimama 👉Unajulishwa unaenda Kushida Vita Yako ya maendeleo uliyonayo. 

Ombea utimilifu wa ndoto hii. 

12:Ukiota Ndoto Magari au Gari La Police linakuja kwako upande uliposimama👉 Unajulishwa Malaika Wa Ulizi Wa Kazi Yako au Huduma Yako. 

Ombea Utimilifu hii ndoto iwe. 

13:Ukiota Gari Mbovu Unaendesha👉Unajulishwa roho ya uharibifu Wa Kazi Zako imo ndani Yako ulishavishwa. 

14:Ukiota Unaendesha Gari barabara nzuri👉Unajulishwa Kazi Yako au huduma itasitawi. 


15;Ukiota Unaendesha Gari Umepakia Mtu👉Unajulishwa Kazi Yako unatakiwa uwasaindie na wegine. 

16:Ukiota Unajifunza Gari Kuendesha👉Unajulishwa Jifunze Kufanya Vizuri hiyo Kazi unayoifanya. 

Ombea Sana hii ndoto

17:Ukiota Gari limekuzimikia mafuta ya Yamekuishia👉Unajulishwa Kazi au Huduma Yako itaishia njiani haitafika kule unataka ifike. 

18:Ukiota Gari Lina ragi Jeusi Gari la bei Kubwa👉Unajulishwa Utafanya Kazi Kubwa na yenye kipato kiKubwa. 

Ombea Sana hii ndoto itimie. 

19:Ukiota Gari la Kijeshi👉Unajulishwa Unahuduma Kubwa ya Ukombozi. 
Hata Gari la Hospital huwa maana moja.
Ombea huduma Yako. 


20:Ukiota gari la Abiria Unaendesha mfano Basi au Kosta nk👉Unajulishwa huduma Yako au Kazi Yako itawasaindia Wengi Sana. 


Nitumie Inbox Kwenye WhatsApp Ndoto ya MAGARI +255710889892

Jumamosi, 19 Julai 2025

SOMO:NIFANYE NINI NIFIKE MBINGUNI

SOMO: NIFANYE NINI NIFIKE MBINGUNI. 
YEREMIA;10:13_17 Mwanzo: Sura ya 7 Na 8 Mwanzo:27:28, 39 Kumb. Torati:14:35

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro
Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
Morogoro Veta Dakawa
Karibuni Watoto Wa Mungu Tu jifunze Tunafanyaje nini nifike Mbinguni au Tupate Kigali na Sisi Kwa Mungu Sababu hatuwezi kumfurahisha Mungu Endapo Swali ndogo kama hili Tutasema Tufanye mema tu ndiyo Tufike Mbinguni Lazima Tujue Kuna visababishi vyakutufanya Tufanye Vizuri Na Tupate kukubalika katika Mbingu. 

Mbinguni ni Makao Ya Mungu Wetu hapa chini ni Sehemu ya kuwekea Miguu Yake. 

Tunaposema "MUNGU" Ni Roho lakini  kazi zake anazifanya Kimwili na kiroho

Mwanzo 1:2 
 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

KUNA MAMBO HAYA YAFANYE ILI  UFIKE MBINGUNI

1;MPENDE MUNGU WAKO. 
Vitabu:Kumb.Torati.6:5 Luka. 10:27

Kumpenda Mungu huhusisha maeneo Manne ya mwili wako. 

1:Nafsi Yako mepende Mungu kuliko dunia

2:Moyo wako mpende Mungu kuliko dunia

3:Akili Yako Mpende Mungu kuliko dunia

4:Nguvu zako Mpende Mungu Kuliko vyote.

5:Roho yako Mpende Mungu kuliko dunia. 

Anasema Yesu  HAYA LUKA;10:27 

Paulo Mtume Katika Warumi Anasema Faida Ya MTU Akimpenda Mungu Hataipendeza Dunia Atafanya kwa kumpendaza Mungu. 

    Warumi 8:8 
 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

      Warumi 12:2 
 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Huwezi Kusema Unampenda Mungu Akili yako haipo pamoja na Mungu au moyo wako haupo kwake au nafsi yako. 


2:MANENO YA MUNGU NA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU YAISHI NDANI YAKO. 

Rejea Haya Maandiko
       1 Timotheo 4:16 
  Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.

Yoshua 1:8
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Ayubu 22:21
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.


MAMBO HAYA YA TAKUWA  KWAKO. 

1:Kuwa Karibu na Mungu. 

2:Njia yako ya maisha kuwa namwelekeo. 

3:Kusikia Maelekezo na yakupasayo ufanye kutoka kwa Mungu moja kwa moja. 

4:Amani na ushindi kwa Adui zako. 

5:Utaongezeka Kiroho nakusimama imara na Mungu. 


3;JITOE KWA MUNGU. 

Matendo;10:1_5

Warumi 6:13
wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.


HAYA YAPO UNAPOJITOA. 

1:Kazi Ya Mungu Itasonga mbele

2;Utahubiri injili kupitia kile ulichokitoa

3:Utabarikiwa mjini na vijijini

4:Mateso na vifungo vitaondoka

5:Mambo Mengi hubadilishwa na baraka mbalimbali zipo kwenye utoaji. 


HAYA NILIYOYAFUNDISHA ndiyo Tiketi ya kwenda Mbinguni kama unataka kufika Mbinguni anza kujifunza Kumpenda MUNGU akilini mwako kwenye moyo wako 


Wapo watu wapo tayari Asiifanye injili iende mbele lakini aende kwa mchumba azini naye na amjegee nyumba au gari amnunulie Hakikisha Unapoweka Alama Ya Kupapenda ndipo hata ukifa moyo wako utatulia hapo ndiyo maana Huwa nasema fundisha moyo wako kuwa mwaminifu Wa zaka Wapo watu akili zao wamezifundisha zikikutana na changamoto kidogo zimuache Mungu na ziache kutoa zaka anaanza kuyafanya yake Mungu anabaki naye mdomoni tu. 


Ndugu yangu Jifunze Akili moyo wako kuiamuru Impende Mungu HAYA yanayokupa kiburi yataishia duniani Ipende kazi ya Mungu. 



Wito

Kama SOMO limekuponya Nifate inbox WhatsApp+255710889892

Niulize Swali nitakujibu

Jumatatu, 7 Julai 2025

SOMO:KUKATALIWA NA BWANA

SOMO: KUKATALIWA NA BWANA
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿
REJEA Vitabu;
 1Samweli:15:25-26
Hosea:4:6

Kuna Watu Wamekataliwa Na Bwana Kama Sauli Pasipo Wao Kutambua Kama Bwana Amewakataa lakini ukisoma habari za Sauli mpaka anakataliwa alikuwa hapendi Neno la Bwana Hasikilizi Baba yake Wa Kiroho Samweli Alichokuwa Akimuangiza Akawa anajiona kwa cheo chake na Elimu yake Anaweza kufanya atakavyo. (1Samweli:15:) 
Pia Mungu alimkataa Hosea Kwa Sababu ya kukataa kwenda Katika maarifa kuwa na Ufahamu Wa kujitambua mwenyewe mtoto Wa Mungu Inawezekana nawewe umekuwa na Tabia za Sauli au Hosea. 

SABABU ZINAZOFANYA MUNGU AKUKATAE. 

1;Kukosa Kutii na Kufata Baba yako Wa Kiroho anachokuambia kinachohusiana na maelekezo ya Bwana. 

2:Kupuuza Neno la Bwana Kukataa Mafundisho nakutaka kuombewa tu kuombewa ombewa kujifunza Neno la Mungu hutaki. 

3:Kuwa MTU Wa kudharau na kuenenda utakavyo kisa cheo chako.

TUFANYE NINI SASA. 

*Tuwe Watoto Watiifu. 

*Tuwe Watoto Tunaofata Maelekezo ya Baba Zetu Wa Kiroho. 

*Tuwe Watoto Tunaopenda kujitambua kujua kwanini Tupo Duniani. 

*Tujue Sababu ya Kuumbwa Kwetu. 

Tambua Mungu Anawatu Wengi Na Huwa Hadekewi Simama Kwenye Zamu yako tii kiongozi Wa Kiroho yaana Baba yako uliyepewa Maana yeye ni kinywa cha Bwana Akitamka kitu kwako utapokea tu.

Jumamosi, 5 Julai 2025

USHUHUDA WA MARTINA 2025 MWEZI Wa 7

USHUHUDA WA MARTINA ALIVYOFUNGULIWA KUPITIA MASOMO. 
====......... =======....... =====........ 
Habari Mtumishi Wa Mungu Pastor Richard..? 
Pole na Hongera Kwa Kazi Ya Kutuombea na Kutufundisha Neno LA Mungu na Ndoa . 
Mimi Ni Mwanao Wa Kiroho Martina Kiando Nipo Kwa Sasa Mtwara Mjini Ninayofuraha Kubwa Kumshukuru Huyu Mungu Kutusaindia Na Kufanikisha Harusi Yetu Salama Kabisa Nashukuru kwa Mafundisho Yako Na Masomo Yako Nimemuona Mungu Akinipigania nimeziona nguvu zake Na Leo Nipo Hapa Kumtukuza Bwana Yesu Kupitia Madhabahu hii ya Moto Wa Yesu Nimefunga ndoa Nimetimiza Agizo LA Mungu Katika Uumbaji wake. 
Lipo Group LA WhatsApp LA Baba Yetu Wa Kiroho Pastor Richard linalenga Maombi na Mafundisho Mimi toka nijiunge limenivusha mengi kupitia Masomo Tu. Ndiyo limenisaindia kufikia Hapa kupitia Maombi ya kuweka Alama Yamenipa Matokeo Makubwa Sana. 

Mtumie Ujumbe WhatsApp Usitume kawaida hataona Tuma kwa WhatsApp hii 0710889892 Muombe Akuunge nawewe ufate unachoelekezwa na kufundishwa utafunguliwa kiufahamu pakubwa mwambie nimepewa namba na Martina Ali kuwa akishuhudia Mahusiano yake yalivyopona mpaka akaolewa kupitia Masomo Yako. 

Pastor Richard Wa Morogoro pia ni Askofu MKUU Wa Makanisa ya Holy Spirit Church Tanzania

Ijumaa, 4 Julai 2025

SOMO: MALAIKA WA SABA RAMIEL

SOMO: MALAIKA  MKUU RAMIEL

Karibu Tu jifunze Leo MALAIKA MKUU RAMIEL huyu ndiye  MALAIKA MKUU WA SABA. 
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro

MALAIKA MKUU RAMIEL ni malaika wa kufufua na kurejesha vitu Katika Hali ya Upya huyu hushughulika na ufufuo wa vitu vilivyokufa kabisa

VITABU REJEA:-EZEKIEL;37  Yo te na VITABU hivi chini

ALIFANYA KAZI NA ELIYA

1 Wafalme 17:21-22
21: Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena.

22: Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.

ALIFANYA KAZI NA BWANA YESU. 

Mathayo 28:5-6 
  5:Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.

6; Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.

ANAFANYA KAZI NA SISI

Wakolosai 3:1-2 
2 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Matendo ya Mitume 4:8-11 
 8:Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,

9: Kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa. 

 10:Jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.

 11:Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.


KAZI ZAKE HUYU MALAIKA RAMIEL. 

1:Kufufua Mambo Yetu Yaliyokufa. 

2:Kurejesha Vitu vilivyopotea. 

3:Kuwa na nguvu ya kufanya Mambo Yetu yawe hai. 

4:Kuyauganisha Yaliyotawanyika au kutapanywa kuvikusanya vitu kuwa pamoja. 

5:Anamsaidia MTU Mambo yake yawe na matokeo chanya.

Anazo KAZI nyingi Kwetu Sana huyu Ramiel ukiona Mambo yako yanakufakufa muite huyu


       NAMNA YA KUMUOMBA. 

1:Baba Yangu Uliye mbinguni Muangizie Malaika Mkuu Ramiel Aje Afufue Mahusiano Yangu UCHUMBA wangu Mimi.... Na... Katika Jina LA Yesu. Ameen
Rudia ×3

2:Malaika MKUU RAMIEL Nayatabiria Maisha Yangu yawe na nguvu ya uhai hayataishi ndani ya mifupa mikavu iwe kazi zangu ndoa yangu biashara zangu nk Katika Jina LA Yesu. Ameen

3:Baba Fufua Mikono yangu Ikawe na nguvu ya Biashara kuzitawala Biashara na kuziendesha Katika Jina LA Yesu. 🙏Amen

TUFANYE NINI

MALAIKA MKUU RAMIEL yupo na atakuwa miongoni mwa MALAIKA WAKUU SABA ATAKUJA NA WEZAKE. 

TUMTUMIE HUYU MALAIKA Kufufua KAZI ZETU MAISHA YETU. 

Wito

Tumia WhatsApp hii ukiwa unaswali au unataka uokoke +255710889892