Jumanne, 25 Februari 2025

SOMO: SHUKURU KWA KIDOGO

SOMO: SHUKURU KWA KIDOGO.

Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro  Kanisa la Holy Spirit church Tanzania. 
Karibu Tujifunze kitu

Jifunze Kuwa Unamshukuru Mungu Vitu vidogo Mungu Anavyokutendea Ipo nguvu mwana wa Mungu Kuthamini hatua mbalimbali za ukuaji wa kiroho kwako na utendaji wa ukuu wa Mungu kwako.

Zaburi;50:14-15
14 Toa sadaka za shukrani kwa Mungu,
timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana,
15 na uniite siku ya taabu;
nami nitakuokoa, nawe utanitukuza

HATUWEZI TUKAWA TUNASUBIRIA MPAKA MAKUBWA TUTENDEWE NDIYO TUSHUKRU.

Tupo watu hata kuomba tulikuwa hatujui Ametufunza kuomba lakini bado hatuoni kama ametenda.

Tupo Watu Tulikuwa hatuna hata wachumba Tumepata Wachumba lakini bado hatuoni hilo kama Ametenda.

Tupo Tuliokuwa Kazini Tumekosa Kibali Sasa Tunakibali bado hatuoni hilo kama Ametenda.

Tupo watu Tulikuwa Hatupendi Neno la Mungu hata kujifunza Sasa hivi mioyo yetu inapenda kujifunza lakini bado hatuoni kama Ametenda.

Tupo watu familia Zetu Zilikuwa Zinateseka Lakini Sasa hivi familia zetu zimefunguliwa lakini bado tunamanug,uniko hatuoni hilo.

HVI VIDOGO TUSIPOSEMA ANSATE BWANA TUNAZUIA MIUJIZA YETU MIGINE.

Mwanangu Hebu Badili Mtazamo Wako Uwe Unashukuru Mungu.
.Soma hili Neno.

1TIMOTHEO:4:4-5
4 Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, 

5 kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba

KILA MABADILIKO YAKO YANAITAJI MUNGU AFANYE UNAPOONA RUDI MAGOTINI NA SADAKA YA KUSHUKURU SEMA BWANA

 Nashukuru Kwa hatua hii Uliyoitenda Kwangu nilikuwa siombi saivi naomba nilikuwa sipati kazi nimepata kazi mtu mwigine akipata kazi privet Bado Anamlalamikia Mungu.

Acha Kuwa Unanug.unika na Kulia Lia Wewe ni mtoto wa Mungu ifikie hatua utambue wewe ni nani katika ulimwengu huu wa damu na nyama. 
Mungu Anasema Mwanangu nijue Vizuri Baba Yako.

Moja ya jambo mhimu ni wewe kujua kushukuru katika kila hatua.

WAKOLOSAI:4:2-3

2 Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. 

3 Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.

TUSIPOTENGENEZA ENEO HILI TUTAKWAMISHA VITU VINGI.

Pia acha kulalamika na kunug,unika Tambua Kazi ya Mungu Kwako anayokufanyia ni kubwa Sana Siyo Jambo la wewe mwanae unayemjua vyema kukata tamaa au kumuacha hili Lichukue litakusaindia 

Mapito na changamoto zisiwe Sababu Za Kufuta mazuri yote uliyofanyiwa na Mungu

Huu mstari hebu urudie rudie utafakari kwa kina maana nasikia sauti inaniambia waambie watu wangu ulionipa uwaongoze kwa Neno la Langu Wawe na Moyo Wa Kunishukuru na Kutambua Najishughulisha na maisha yao kuliko nguvu zao na akili zao na Elimu zao Japo hawaoni wananilalamikia Sitendi kwao.

AYUBU;22;21-22

.21 “Mjue sana Mungu ili uwe na amani,
ndipo mema yatakapokujia.
22 Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake,
na maneno yake uyaweke moyoni mwako

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni