Ijumaa, 28 Februari 2025
SOMO; MAHUSIANO YANA LUGHA MBILI TU.
Alhamisi, 27 Februari 2025
SOMO: NI BORA UCHUMBA ULIOVUNJIKA KULIKO NDOA ISIYO NAAMANI MILELE.
Jumanne, 25 Februari 2025
SOMO: SHUKURU KWA KIDOGO
Jumatano, 19 Februari 2025
MAOMBI YA USIKU WA MANANE 2025
MAOMBI YA USIKU WA MANANE LEO.2025
SAA;6;00Usiku mpaka
Saa;10:00Alfajiri
Ukiamka Huu Muda ingia Vitani Ombea kila Jambo unaloona haliendi Waunge na rafiki zako Kwenye Group wanaopenda masomo na Maombi unawapa utaratibu kabla hujawaunga
Karibu Sana Tambua Usiku huwa ndiyo muda mzuri Wa Mungu Kuwashughulikia Adui Zako na Matatizo yako kuyashughulikia.
HAKIKISHA UMEOMBA TOBA KABLA HATUJAANZA KUPINGA NA KUSHAMBULIA
MSTARI WA KUSIMAMIA Kutoka;11;4
4 Kwa hiyo Mose akasema, “Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Panapo usiku wa manane Mimi nitapita katika nchi yote ya Misri.
Rudia kusoma chukua point hii Mungu Apite kwako
TUTAOMBEA MAMBO MATATU
1;Roho Ya Uzuizi Kwenye Wokovu Wako.
Ulishawahi Kujiuliza Kwanini mliokoka wengi wezako walishaacha Wokovu wakawa watumwa wa dhambi wewe unaendelea vizuri nakujitakasa mara kwa mara.
Ipo hivi Unapookoka Shetani huandaa roho chafu mbalimbali za kuhakikisha Huendelei Mbele Na hutumwa vitu mbalimbali vya kukatisha tamaa na kupelekea uache wokovu.
OMBEA WOKOVU WAKO UWE IMARA USIJE UKAWA MSINDIKAJI.
2;Roho ya Kuzuia Kutenda Matendo Mema.
Ipo roho hupandikizwa ndani yako unapokuwa umeamua kutembea na Mungu Ambayo itakufanya tu njia zako zisiwe Sahihi hata kama umeokakaje Matendo yako yatakuwa na udhaifu Tu.
Ombea Matendo yako Yawe na Kibali Kwa Mungu.
3:Roho za Mafatilizi ya Hatua Unazokuwa Unachukua
Mtoto wa Mungu Zipo roho Hufatilia Kila steji unayotaka uifanye omba shugulikia.
Ndio Maana Unaweza ukaanzisha Jambo unaamua kuliacha au Uchumi unapigwa kiasi kwamba hata hela ya Kula Unaanza Kukopa ule.
Jitaidi Kuwa Siriazi Na Upende Kuongezeka Kiimani Sikiliza Muongozo wa Maneno Roho Mtakatifu anayokupa wakati ukiomba usiku.
FAIDA ZA KUOMBA USIKU WA MANANE
Matendo;16;25-26
1;Maombi ya Usiku wa Manane Yana nguvu yakukufungua Matatizo yako Mengi.
2:Maombi Ya Usiku Ni Tulivu unakuwa husumbuliwi upo uweponi.
3:Mungu hupita kuwatandika adui zako vibaya mno.
4;Unapata mume au mke kupitia kuomba usiku wa manane.
Samsoni na Delila walipatana Usiku wa manane.
5;Unajimarisha kiroho na Kimwili katika Vita za Kiroho.
6:Unakuwa na nguvu ya kuomba Sana..
Taja nawewe unazozijua
Omba nasi Usiku wa Manane kila Siku.
.
HOLY SPIRIT CHURCH TANZANIA ILIPO NASISI TUPO HAPO.
Moto Wa Yesu Uwake Zaidi ya Jana.
2025 Tunatembea Kibabe
Mathayo;11;12
Shirikisha na wengine muombe Pamoja na rafiki zako.
.Mawasiliano na Bishop Richard Mwenyewe 0759861768 au Tigo 0710889892