Jumatatu, 25 Novemba 2024

SOMO:, KUTAFUTA NA KUPOTEZA UNACHOPATA HUFANYI LA MAANA

SOMO;ROHO YA KUTAFUTA NA KUPOTEZA UNACHOPATA HUFANYI LA MAANA.

Kuna Watu Wanayonguvu ya kutafuta na Kupata Pesa Lakini Hawana nguvu ya kutumia Pesa yao ikawapa faida. Hii ni roho hatari imekuwa ikitesa Watu Wengi Sana Wapo wengine Wanapata kazi mwaka mmoja Ameshapoteza Kazi Tena. Wengine wamepoteza wachumba wao wengine ndoa  zimepotea. Nk.

KUTAFUTA=Ni kujishughulisha na kitu.

KUPOTEZA=Ni kutumia ulichokipata katika mambo ambayo hayana Maana.

Karibu Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kutoka Kanisa la Holy Spirit Church  Tanzania 

        MISTARI YA KUSIMAMIA TUSOME.
  Nehemia:6:16  Isaya:44:12

            Muhubiri:3:6
6 wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,
wakati wa kuweka na wakati wa kutupa

          Kumb.Torati:15:9
9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia Bwana dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.


KABLA YA KUOMBA FANYA HAYA.

1:Kwanza Uwe na Utayari kuikataa hali ya kupoteza.

2;Ingia uombe hakikisha unatamka Maneno


➖"Natafuta Pesa nitazitumia Sitapoteza Pesa ikae mikononi mwangu kuanzia Leo Katika Jina la Yesu.Amen 

➖Nakataa kuwa mtumwa wa kutafuta Pesa halafu hazikai mikononi mwangu Sasa ninaamuru Pesa nitakayoishika kuanzia mwezi huu Katika Jina la Yesu.Amen 

➖Roho ya Kupoteza Achia Kazi yangu achia Uchumi wangu achia ndoa yangu achia Katika Jina la Yesu.Amen 

➖Baba Yangu Ninaomba kila kifungo kilichounganishwa ndani yangu kinifanye niwe napoteza vitu kiniachie katika Jina la Yesu.Amen 

Endelea Kuombea kila mazingira Ambayo umekuwa ukipoteza wapo wengine wanashika mimba zinaharibika Wengine Wamepoteza Afya zao Wapo wengine wachumba wamepoteza hata mawasiliano hakuna Sasa basi Shughulika Bila kuchoka hii roho ikutoke.

UTAJUAJE UMESHAFUNGULIWA.

Hutapoteza Vitu utakuwa unaona faida.
Waliokukopa watakulipa Madeni.
Utashika mimba na haitaharibika
Utafanya kazi Faida utaona.

HITIMISHO 
Unajua watu wengi mikono yao  imefungwa wanatufuta hawatumii kuleta faida katika kile walichokitafuta.
Basi Tuombe Mungu atufungue roho za kupoteza Tusiwe Tunapoteza.


Tuma ujumbe WhatsApp Uombe kuungwa kwenye group hili la maombi na mafundisho +255759861868


Jumatano, 20 Novemba 2024

SOMO; Mungu Huzingatia Haya Anapojibu.

Somo: MUNGU HUZINGATIA YAFATAYO ANAPOFANYIA KAZI OMBI LAKO.

Hakikisha hizi CV unazo kabla ya kuwasilisha Mahitaji Yako mbele Zake.

Unajua Watoto Wa Mungu Wengi na Watu Wengi Hufikiria Mungu Ukimuomba Anajibu tu hazingatii chochote Maana Wajibu Wake Kujibu. Hapana Mungu Hayuko Hivyo Mungu Yupo Makini Sana Kumsikiliza Mwanao Anapomuita Kuliko Eneo lolote Sasa ili Amjibu Katika Maombi Yake huzingatia Yafayo:
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
1:KWANZA WEWE UNAYEMUOMBA AFANYE KITU AU AKUJIBU MAHITAJI YAKO UMEFANYA NINI KWAKE..? YAANI UNAALAMA NGANI UMEFANYA KWA MUNGU?

Swali hili jiulize na ufikirie wewe unaomba Mungu Afanye hiki Wewe mwenyewe mwizi wa zaka hujawahi nunua kanisani hata Tenzi za rohoni hata viti hata kushonea watumishi suti au wajane na Yatima. Mungu Akiutazama huu moyo wa hivi Anaacha Anamtafuta mtu Ambaye hufanya kitu kwake Yeye huyo huwa Mwaminifu kujitoa kwake kusaindia wengine nk.
.
REJEA HIVI VITABU UJIFUNZE KITU.
MATENDO;10...Hii habari ya mtumishi mmoja Mkuu wa majeshi Serikalini yeye na familia yake walivyokuwa watoaji

 MATENDO;9:35.....Hii habari Ya Bint mmoja Fundi Cherehani Kipato chake cha chini lakini alikuwa mtoaji.

1Samweli:1 ....Hii Habari Ya Wazazi wake Na Samweli walivyokuwa wakijitoa kwa Bwana.

➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖

2:JAMBO LA PILI MUNGU HUANGALIA NAMNA YA UWASILISHAJI WAKO  WA MANENO.

Hatuongei ovyo ovyo Bila mtiririko Tunapoomba mbele Za Mungu  Tunapaswa Tutambue Tunaongea na Nani na Maneno Yetu Yanatakiwa Yawe ni Kiwango Kipi cha Hekima na Unyenyekevu  na Kujishusha Siyo unaongea naye Huombi mbali unalia tu au Unaenda Kwake Umenuna unaanza kumtupia lawama na kumfokea Kinywa chako kikontoro mtoto wa Mungu Usichukulie kuomba ni rahisi rahisi mpaka ulete majibu.

VITABU REJEA 
Soma Habari Ya Hanna alipokuwa Anaomba 
1Samweli:1:12-20

Soma hata Mitume Walivyokuwa wakiwasilisha maneno wakiwa wanaomba
Matendo:1:23-26

WAKOLOSAI;2:1-5
1;Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi..

 2 Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe

, 3 ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa.

 4 Nawaambia mambo haya ili mtu yeyote asiwadanganye kwa maneno ya kuwashawishi. 

5 Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.


3:UKAAJI WAKATI UKIWA UNAOMBA MUNGU.

Umekaaje Kaaje Unapokuwa Unaomba Au Wewe unajua kukaa tu. Lazima ujifunze ukaaji wako ukiwa unaomba kaa kwa nidhamu na kwa heshima Sababu unaenda kuzungumza na mwenye umri kukuzidi Elimu kakuzidi Uchumi kakuzidi kila kitu Amekuzidi Kwanini ukose Adabu. Wapo watu wanapoomba ukaaji wao utafikiri hawapo kwenye kuomba Anaomba huku Ameshika hiki mara amekaa ovyo. Kama umepiga magoti piga kwa heshima. Kama ni kusimama simama kwa heshima.

REJEA KUSOMA;
➖➖➖➖➖➖➖
Matendo:20:36-38

DANIEL:6:10
 10:Basi Danieli alipofahamu kuwa amri ile imetangazwa, alikwenda nyumbani kwenye chumba chake cha ghorofani ambako madirisha yalifunguka kuelekea Yerusalemu. Akapiga magoti na kuomba mara tatu kwa siku, akimshukuru Mungu wake kama alivyokuwa akifanya mwanzoni. 


HITIMISHO 

Acha Niseme Kwamba Ni Muhimu Sana Kujua hili Sababu Unaweza Ukawa Mtu wa Kuomba maombi Yasiyo na Matokeo ikafikia hatua ukaanza kumlaumu Mungu wetu nakuona kama Anaubanguzi Anajibu Wengine kumbe wewe mwenyewe upo nje ya Kanuni Zake Mungu katika Eneo la Maombi.

Kama upo nje ya Group la Maombi na Mafundisho mtumie ujumbe WhatsApp Pastor Richard Akuunge +255759861768


Shirikisha ujumbe huu kwa kuutuma kwa watu wengi zaidi mpaka umfikie Anayependa Kumlaumu Mungu hamjibu.

NAKAMA UNAFANYA HAYA MUNGU HAJAJIBU ELEWA NI LA MUDA LAZIMA AJIBU SABABU UNAALAMA KWAKE UNAFANYA VITU NA KUJITOA KUSAPOT KAZI YAKE HAUFURAHII UKIONA INATUKANWA AU WATUMISHI WAKE WAKILALA NJAA UNAJITOA KUWALISHA.

Jumapili, 3 Novemba 2024

SOMO:MAOMBI YA KUOMBEA HAJA YA MOYO WAKO

            "DARASA LA MAOMBI "
=============================
SOMO:MAOMBI YA KUOMBEA HAJA YA MOYO WAKO.

Kila mtu huwa Anamatamanio Ya Vitu Anataka Avipate Lakini Hawezi Kuomba Akavipata Sasa Kupitia Darasa hili la Maombi utajifunza uombaje

MUNGU HUZINGATIA 
1;Uwasilishaji wa Maneno.
2;Ukaaji na Uaminifu Wako kwake.
Hakikisha hivi vitu uwe navyo ukitaka unaomba unaleta majibu.

Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Tunasimamia Mistari hii.Tusome.
        MITHALI;30;7-8
7 “Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana;
usininyime kabla sijafa:

8 Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo;
usinipe umaskini wala utajiri,
Bali unipe chakula cha kunitosha kila siku

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBA;

1:Omba Kitu Ambacho ukikipata hutamuacha Mungu Sababu kuna Vitu vingine ukivipata tu Wewe Vinakutenga na Mungu.

2;Omba Kataa Umasikini na Kila hali inayofanya Watu Wakudharau.

3:Omba Uwe na Upendo Wa Kiasi kwa Kila Eneo.


NAMNA UTAKAVYOOMBA;

MFANO : 1:UNAOMBA UOLEWE/UOWE.

👉Bwana Wangu Mwokozi Wangu Umenijua toka tumboni mwa mama ukanipima uaminifu wangu kwako katika utoaji wa zaka Na Sadaka Nimekuwa mwaminifu pia hata dhambi ya kuzini nimeishinda Bwana Wewe Mwenyewe Unaona Nilivyosimama Kujitunza Nipate Kibali Machoni Pako Mungu Wangu Niletee Mume Wangu Ubavu wangu au Niletee Mke Wangu Nyama katika mifupa yangu Muda wa Mimi Kuwa na Mwezangu umefika mfungulie Miguu Anifate Katika Jina La Yesu.Amen 

Rudia ×6
ANGALIZO:
Hakikisha Unapoomba uendane na maneno yako uwe kweli zaka umesimama mwaminifu uwe kweli huzini. Mungu huwa hajibu kwa mtu asiyemwaminifu kwake.


MFANO 2; UNATAKA UPATE KAZI.

Baba Yangu Bwana Mwenye nguvu na Mamlaka Nashukuru Kwa Nafasi hii umenipa nione Nami Napendwa nawewe nimeomba kazi Baba Nimeomba Kazi Baba Naomba Jina Langu Lisikosekane Jina langu mimi mwanao Ni Richard Julius Kushoka Ndiyo hivyo nimejaza kwenye usaili Tuma Malaika Wako hili Jina Walipitishe Kila Eneo litapoonekana nami nakuapia Mungu nikipata Kazi Nitakuwa Mwaminifu Sana Tena Sana Kwenye hii Madhabahu Ya Moto Wa Yesu.Amen 

Rudia ×3
ANGALIZO:
Hakikisha Ukipata Kazi Huachi Kutoa Fungu la Kumi Unakuwa Mwaminifu kupita Kawaida.


MFANO;3 KUOMBA UWE NA UZAO YAANI UPATE WATOTO.

👉Shika Tumbo lako Ongea maneno haya kwa mwanamke.

Wewe Tumbo Nakuongelesha uliambiwa nikiolewa tu ulete Uzao Uijaze Dunia ulete Watoto Kwanini mpaka Sasa huna uzao Nakuamru kama kuna anayekuzuia au Amekufunga usinipe watoto nakufungua kwa Jina la Yesu. AMEEN 


👉Mwanaume Shika Kiuno Kama Huzai.

Wewe Kiuno changu Nakuambia kuanzia Sasa ufunguke ukazalishe Mbengu zilizopo ndani yangu zitungishe mimba kila kinachozuia mimi nisiitwe Baba Kiachie Katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×1
ANGALIZO:
Hakikisha unatamka nilivyoelekeza Kwa kila jinsia omba mara kwa mara sio uombe siku moja tu.


MFANO:4 KUOMBA UPATE MTAJI WA BIASHARA 

👉Bwana Yesu Nakuomba uwaruhusu watu uliowadaa wanipe mtaji waje nimechoka kukaa bila kukutolea zaka najiona kama ni mwenye hatia nipe mtaji Baba Uone uaminifu wangu nitakavyosimama kuwa mwaminifu pia unipe na wateja wengi Sana. KATIKA Jina la Yesu Ameen 

        OMBEA WATEJA;
Baba Yangu fungulia Wateja muondoe kwenye mlango pepo anayezuia wateja wasiingie Bwana Weka Malaika wako Awe Anawavuta Wateja Waje waje Waje Kwa Wingi Katika Jina la Yesu.Amen 

ANGALIZO:
Kila uendapo kwenye biashara ombea upate wateja wengi.

MFANO:5 OMBEA MAHITAJI YAKO MBALIMBALI.

Mahitaji yapo mengi Kwa hiyo Ni Vyema Zingatia Uwasilisha wa maneno yako Kwa Mungu unapoomba pia kuwa mwaminifu kwa Mungu acha kuwa mdanganyifu kwa Mungu.

Mfano:Kuomba upone magonjwa;
Baba Yangu Nakuomba niondolee magonjwa mwilini mwangu Baba nitazame mwanao kwa jicho la huruma nipo chini ya miguu yako kwanini unaruhusu magonjwa mwilini mwangu kumbuka nilivyomwaminifu katika madhabahu hii ya Moto wa Yesu sijawahi kuacha kukutolea Zaka na hii ndiyo Madhabahu uliyonipa Bwana Kumbuka nimenunua vyombo vya mziki kanisani nimenunua viti yote hii ni uaminifu na Upendo wangu kwako Baba Kumbuka niliyoyafanya kwako naitaji niendelee Kufanya Nakuomba Uniondolee mateso haya mwilini mwangu Baba nitafanya kwako zaidi ya niliyoyafanya kwako Ansate Mungu umesikia Maombi Yangu Nipe nguvu Sasa kwenye mifupa yangu Mwili wangu nitembee nifanye kazi zangu pasipo na magonjwa nikienda Hospitali wasione tatizo tena nafunga kabisa kwa Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×5

ANGALIZO 
Hakikisha unapoomba uwe kuna vitu unafanya kwa Mungu iwe kama Sababu ya Mungu Akuponye ili uendelee kufanya mengi kwake kama huna Sababu ni ngumu sana kumshawishi Mungu.
Kumbuka Ezekiel alifanya kitu Akaponywa magonjwa.



Natumaini Kuna Jambo umejifunza Naomba ukiwa unaswali niulize inbox WhatsApp number +255759861768

Shirikisha wengine