Jumanne, 28 Mei 2024

MAOMBI YA KUJITENGA VISHAWISHI

MAOMBI YA KUJITENGA NA VISHAWISHI VYA DHAMBI MAKAZINI;

Kuna Watu Katika Ulimwengu Wa Roho Walishauganishiwa mitengo ya Kuwa Wana nasa kupitia Wanawake wa maofisini au Wanaume Ambao hawa Wanakuwa Wanawashawishi Kuingia Katika Dhambi Nao Kwa Kuwa Ufahamu wao Umefungwa Wanaingia Kwenye mtengo wakishazoeana inawapelekea Wapoteze Kazi Inawapelekea Wawe watumwa wa kutumikia dhambi kulinda kazi au nafasi zao. Hii kama wewe ni miongoni mwao haya maombi yaombi unayeishi kazini kwa utumwa wa dhambi Omba haya maombi.

   MISTARI YA KUSIMAMIA 
🍏🍏🍏🍈🍈🍈🍈🍈🍈🍏🍏🍏
Mithali 1:10
[10]Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, 
Wewe usikubali. 
πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’
Mithali 7:21
[21]Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, 
Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. 
πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰
Matendo ya Mitume 6:11
[11]Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu. 


MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUOMBA HAYA MAOMBI 

1: Unatakiwa uwe unaipitia hali ya Vishawishi na Makwazo Kazini

2:Utaandaa Sadaka Yako Kiasi chochote Ukimaliza Maombi utaituma unanipigia.

3: Utaomba Siku moja tu. Muda Wowore Utao utenga.



 JINSI YA KUOMBA  OMBA HIVI 
🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝🏝


1:Nakama Anga la Kazini hapa Kila Kishawishi Ninachokutana nacho hapa kazini ninakataa na Sikubali kuwa nakutana na Watu Wanaonidharau Katika ofisi yangu kila atakayeniona Aniheshimu na Asinishirikishe Dhambi au Kupewa maneno yanayonitenga na Mungu wangu Katika Jina la Yesu.Amen 


2;Shika kwenye Paji la Uso Omba hivi
Ninaomba Bwana Unipe Kibali na Nguvu ya kuitawala ofisi yote kuanzia uongozi wa chini mpaka juu kila idara ninatawala Katika Jina la Yesu.Amen 


3.Mimi Sitaki vita au Kufokewa fokewa na kutumwa tumwa kazini nataka niheshimike na kuanzia Leo Sitafatwa kutongozwa au kutongoza Watu Wa hapa kazini kwangu naiweka heshima ya majukumu yangu ya kazi kila roho inayotaka Ichukue heshima ya kazi yangu kupitia Katika Jina la Yesu.Amen 

  4: Endelea Kuomba haya  Maombi Kadiri 
Roho Mtakatifu Anavyokuongoza kuombea eneo la kazini kwako



SADAKA YAKO IOMBEE.

Kupitia hii Sadaka ikaongeaa kwa habari ya ukombozi eneo la kazi yangu kila Kishawishi sitaki kunaswa na dhambi zinazotumwa na Adui kupitia kazi niliyonayo naitoa katika madhabahu ya Moto Wa Yesu kwa Jina la Yesu.Amen 


TOA KWA 

M-PESA 0759861768

TIGO PESA 0710889892

HALO PESA 0628355985

CRDB BANK 0152361572400

JINA; RICHARD JULIUS KUSHOKA 

Kisha unipigie uniambie umeomba haya maombi 





Alhamisi, 23 Mei 2024

SOMO: SI SAHIHI KUFANYA HAYA MBELE ZA MUNGU.

:::::"""""DARASA LA UCHUMBA::::""""""",,,,,
===============================
SOMO: SI SAHIHI KUFANYA HAYA UNAPOTAKA MWEZA

Tusome Mwanzo:24 Yote

Karibu Ujue mambo Ambayo Siyo Sahihi Kuomba mke au mume mbele za Mungu ukiwa navyo Akilini mwako vitakupa majibu siyo sahihi ukivishikilia Hivi vitu.
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

Tusome hii misitari.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mathayo 1:19
[19]Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 


Mwanzo 24:28
[28]Basi yule msichana akapiga mbio, akawaambia watu wa nyumba ya mama yake mambo hayo. 


Mambo Haya Siyo Sahihi Kuomba Huku Ukiwa navyo  Mbele Za Mungu Ukitaka Akupe Mume kutoka Kwake.
πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸ‰πŸŒ³πŸŒ³πŸŒ³

1; KUOMBA  MAOMBI YA KUPATA MKE AU MUME KUTOKA KWA MUNGU HUKU UKIZINI


Yaani ukiwa upo katika kutafuta mme au mke wa kutoka kwa Mungu lazima uwe mwaminifu Wa kuacha kuzini Na Kuwa mwaminifu kwa Mungu kuepuka dhambi hii 

Lakini Usipoepuka Kuzini Na Ukawa unaomba nakufunga Mungu Akupe mke au mume Shetani atafulululiza kuwaleta watu wake ambao watakuja na Mawazo ya Kuzini nawewe tu na ukifanya hivyo wanakuacha.

Mithali:6:32 Ukizini unabembelea mikosi laana na hata kukosa thamani ya kuitwa mtoto wa Mungu tena.


2.KUOMBA HUKU UKIWA UMEWEKA MTU AKILINI.

Usiende Kuomba huku mawazo yako Kuna kijana au Bint Kanisani Anakuvutia kwa kuwa yupo karibu nawewe au anakuchangamkia ukionana naye au Kuanza Kuomba Mtu fulani Akuowe Huku ukimtaja Jina lake Au Kuanza Kumwambia Kijana Akuowe Ambaye hujaomba umekaa tu mawazo yako yakakutuma kwa kuwa umeona yupo kwenye Group la maombi linaloongozwa na Pastor Richard ukajua sahihi omba kujirizisha.

Kama Wewe huombi ni rahisi Shetani kukuletea mtu ambaye siyo sahihi kwako.


3:NI MUHIMU UWEKE VINGEZO KAMA ISAKA UNAPOOMBA.  USIOMBE BILA VIGENZO KUWEKA ILI UJUE KIURAHISI


Ili iwe rahisi Kwako Kujua maombi yako Mungu Amekujibu Ni Muhimu Kuweka  Viashiria fulani au kuweka Alama endapo huyo mtu ni wako Mungu Afanye vitu hivi na hivi.

Ukiona Mungu Amevifanya hivi vitu ujue huyo ni sahihi ubavu wako taba naye usimuache.
Ukiona hakuna haijatokea ulivyosema achana naye maana si ubavu wako. Yupo anakuja uliyeandaliwa endelea kuomba.


4;KUWA NA BABA YAKO WA KIROHO ALIYE VIZURI KIROHO ILI AKUONGOZE VIZURI NA HAKIKISHA UNAMTII NA KUFATA MUONGOZO  USIOMBE MAOMBI UKIWA HUNA BABA.

Hii watu wengi hupuuza wanakuwa na wachungaji wengi au mababa wa kiroho wengi Unajikuta hata Mungu Unamvuruga Eleweka Uwe na Baba yako wa Kiroho utakayeshuhudiwa ndani yako huyu ndiye atakuwa baba yangu hata niende wapi nitamshirikisha mambo yangu yeye nitaomba ushauri nayeye ndiye atakayeniombea Usiwe wa kuombewa ombewa na kila mtu anakushika kichwa chako uwe na mtu mmoja Baba mmoja kwigne kasali kisha toka ukiambiwa wenye matatizo pateni mbele kama siyo kwa Baba yako Usitoke 

Heshimu mafuta na Upako alumnae Baba yako unaweza kukuvusha Mungu kamwamini ndiyo maana akakupa akuongoze kiroho awe anakuombea.

Eleweka utulie Sehemu moja Fungu la kumi toa kwa Baba yako wa kiroho na Siyo kila sehemu unatoa fungu la kumi.


5:WEKA RATIBA NA UKOMO WA MAOMBI 
USIOMBE BILA MUDA


.Unatakiwa uwe na muda maarumu uliotulia kuombea hili lakini unapoombea

Anza kutoa fungu la kumi kwa huyo Baba wa kiroho mshirikishe kila hatua Na Ufate Muongozo wake na Atakavyokushauri Endelea kuomba mpaka Ukomo wa Muda uliojiwekea.

Ukifika huo muda hujaona majibu endelea kushukuru kwa Mungu na uache kuombea tena hilo baadala yake Uwe mwaminifu wa fungu la kumi kwa Huyo Baba yako wa kiroho na kuomba mahitaji mengine.

Mungu atakuja kukujibu Maombi yako na ukijibiwa utaona viashiria vyote ambavyo uliziweka huyo mtu anavyo  utaelewa kwa haraka.


USHAURI WANGU KWAKO.

Changua kwanza uwe na Baba wa Kiroho Uanze kufata muongozo wa Baba yako wa kiroho pia kumshirikisha Changua Baba atakaye kulea kukuongoza kukusikiliza na unamwelewaa anapokufundisha pia Ambaye huyo ndiyo atakufikisha kwenye majibu yako na uhakikishe Uaminifu wa Fungu la Kumi kwake.

Baba wa Kiroho hata akiwa yupo mbali nawewe lakini unaweza kuongea naye akakushauri kukusikiliza ukamwelewa Basi huyo atakufaa 

Huwezi Kwenda Kiroho Kama humsikilizi Baba yako wa Kiroho Mungu aliyekupa kama utapata wa nje na unaposali ni vyema ukamuomba nataka uwe Baba yangu wa kiroho nakuanzia Leo nitatoa zaka kwako.

Ukifanya uchanguzi wako uwe na msimamamo usiyumbe yumbe utulie huko

Ikitokea kanisa unalosali linakulazimisha utoe utatumia Hekima maana Wengi Fungu la kumi hulichukua kimwili Utakachofanya mwezi huu utatoa kanisani mwezi ujao unatoa kwa Baba yako wa kiroho ili kutembea na Madhabahu yako ujue ulipo siyo Madhabahu yako.


HITIMISHO 

Ansateni Sana Kwa Masomo haya najua umepata picha Ya vitu unaweza ukawa una unafanya siyo sahihi

Nifate inbox uniulize Ambapo hujaelewa 



Jumatano, 22 Mei 2024

SOMO; USIANZISHE MAHUSIANO UKIWA NA STRESS

πŸͺ🐫DARASA LA UCHUMBA πŸƒπŸ‚
πŸŒ΄πŸŒ΄πŸŒ΄πŸπŸπŸπŸπŸπŸ‹πŸ‹πŸ‹πŸ‹πŸ‹

SOMO: USIINGIE KWENYE MAHUSIANO UKIWA NA STRESS.
Mithali;12;1-3

.Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa 

             Zaburi 121:7-8
[7]BWANA atakulinda na mabaya yote, 
Atakulinda nafsi yako. 

[8]BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, 
Tangu sasa na hata milele. 


Kuna Hiki Kwenye Mahusiano Kitambue Usianzishe Mahusiano ukiwa upo unapitia stress au umetoka kuumizwa au kuna vitu vinakuvurunga.

Hii ni Kwa Ajili ya Usalama Wako Wa Kiakili na Hata Kiufahamu .

HAYA YAFATAYO HUJITOKEZA KWA ANAYEJICHANGANYA.

1;STRESS NDIYO ZITAKUWA FIMBO ZA SHETANI KUZITUMIA.

Mara nyigi ukiwa umetoka kujeruhiwa au unavitu vinakusumbua akilini akuanzisha Mahusiano Tengemea uchumba wenu utakuwa wa ugomvi au kukosa Amani Sababu umeingia Kwenye uchumba na maroho ya kujeruhiwa na maumivu mbalimbali shetani atakuhubiria STRESS zako kwenye uchumba mpya nao utavunjika.


2.USIZITUMIE STRESS ZAKO KWA MCHUMBA WAKO. ULIYENAYE.

Matatizo yako au changamoto ulizowahi kuzipitia au unazozipitia usianze kumweleza mchumba wako ambaye hajakuowa au hujamuowa Usiaze Kumtwika madeni yako au Kodi Akulipie au Karo hivyo hivyo mwanaume Bint kama hujamuowa usiaze Kuchukua Pesa au Kwenda kwenye Nyumba aliyopanga Bint au anapokaa Usiaze kumwambia Akupe mtaji 

Hakikisha Akuowe au uolewe naye ndiyo uanze kumuomba hela na kufanya mambo kama mke na mume.


3.NAFASI YA MKE AU MUME USIAZE KUITUMIA KWENYE UCHUMBA. 

Mwanamke hurusiwi kwenda kwa kijana ukamfulie nguo au ukampikie au Kwenda Kumtandikia Kitanda chake Na Wewe Kijana Wa Kiume Usiende kwa Bint Ukaanza kumhudumia kumgharamia wakati siyo mkeo na hujui wewe ndiyo utaishi naye.

Hayo yafanye ndani ya ndoa


4:USIMKATIE SIMU MCHUMBA WAKO AU KUTOKUJIBU SMS KISA UNAPITIA KIPINDI.

Usianze Kuvunja uchumba wako au Kuharibu furaha ya Mahusiano yako kwa matatizo au changamoto zinazokuvurunga hasira ukazirundisha Kwa akupenda ukaacha kuongea naye au kukata simu zake wakati yeye anakuwa hajakukosea lakini kazini umevurungwa unaleta hasira kwenye uchumba wako.

Utavunja Mahusiano yako mwenyewe ukiwa hivi.


5; UWE NA MSIMAMO USIWE MLEVI WA UCHUMBA. 

Mlevi huyumba yumba haeleweki amesimama au anaenda kuaguka chini Wewe unatakiwa uwe na msimamo mkali Wa kuolewa siyo kuchezewa au Kutumiwa na shetani kwa dhambi za kuzini mbali Mungu akutumie ufanye Tendo la Ndoa

Hakikisha huvunji uhusiano wako na Mungu kwa Kuzini na mtu asiyejulikana kwa wazazi.



TUFANYE NINI

Uchumba Unaitaji Uanzishe Ukiwa hujavurungwa akili ikiwa ipo vizuri na unao utimamu wa kiafya na kiakili Sababu unaenda Kuandaa Ndoa na Familia Bora ya Baadae.


WITO

Niulize inbox au tuma kero yako inbox nitakujibu pia share kwa watu ujumbe huu.

Jumatatu, 20 Mei 2024

SOMO: MAISHA YA NDANI YA NDOA

    .,,,,,.SHULE YA WANANDOA,,,,,,
$$$===================$$$$$$


   SOMO:MAISHA NDANI YA NDOA  


Habari Wanandoa  Tuongee+18 Nawakaribisha Somo hili Ambalo Limenijia Usiku huu niweze kufundisha Wanandoa Mambo Sita yanayotufanya Ndoa Tuishi na Kuifurahia na Kuiongoza vyema Bila Matatizo au Misukosuko Tunaotaji Kukubali Neno liingie kwenye maisha ya ndoa zetu 

Biblia Inaangiza namna ya Kuishi ndani ya ndoa.

Naitwa Pastor Richard Mwalimu wa Wanandoa Nipo Morogoro Veta Dakawa Kutoka Kanisa la Moto wa Yesu.


TUNAISHI NDANI YA NDOA KWA KUFATA HAYA 


1;KWA HEKIMA; (Mithali;14;1)


Ili ndoa Zetu Ziwe Salama Tunaitaji Mungu atujalie hekima ya hali ya juu sana Ndoa Siyo uchumba ndoa siyo kitu rahisi kama huna Hekima Nikushauri tu ni bora usiowe au kuolewa sababu utaumia sana ukiingia ndani ya ndoa huna hekima.

TUSOME ANDIKO..

Mithali 14:1
[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; 
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. 


Lishike hili Angizo la Kwanza liwe kwenye ndoa yako.


2.KWA AKILI SANA; (1Petro:3:7)

Wanandoa Pekee Wanaitaji wawe na Akili ya kujuana haraka kumjua mwezako mapungufu yake kujuana tabia zenu ukiwa ndani ya ndoa harafu mwezako humjui au Akili zako mpaka zishutuliwe ndiyo ujielewe upo ndani ya ndoa ufahamu wa kujiongeza mwenyewe huna uwezo wa kufanya vitu huna Upo upo tu Ndoa hii kwa vyovyote itakuwa na shida.

Ukiingia ndani ya ndoa sababisha kuleta utofauti wa maisha yako kabla hujaowa na baada ya kuowa.

TUSOME ANDIKO:

1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu


3.KWA KUTII (Waefeso;5;22)

Utii huwa unanguvu Sana Mwanamke Mtii mumeo na kumsikiliza unapoingia ndani ya ndoa ukianza kiburi na jeuri Mtaanza Kupisha na kugombana Kumbe neno utii mumeliondoa Ndani Ya Ndoa. Mumeo akisema hapendi matumizi mabaya ya Pesa uelewe kuna vitu unavinunua hivina maana kwa wakati huo basi msikilize uache mara moja.


TUSOME ANDIKO:

Waefeso 5:22
[22]Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 


4;KWA TENDO LA NDOA;(1 Wakoritho; 7:3)

Mwanamke ukiwa ndani ya ndoa ni wajibu wako kumpa tendo la ndoa mumeo muda wowote ule anapoitaji hali kadhalika na Mwanaume mkeo akiitaji tendo la ndoa ni wajibu wako Kumpa tendo la ndoa mkeo Asiwepo kati yenu Anayemzuia mwezake katika haki yake ya ndoa Na hii itawafanya Ndoa Yenu I imagine Zaidi.

TUSOME ANDIKO:

1 Wakorintho 7:3
[3]Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 

.
5.KWA UPENDO MWINGI (Waefeso:5;25-29)


Ni wajibu wa mke na mume upendo kwao kupendana katika viwango vikubwa chochoeni Upendo ndani ya ndoa Msiupuguze Upendo fanyeni vitu mnavyojua vinawapa upendo zaidi na Kukaa ndani ya upendo.

TUSOME ANDIKO 

Waefeso 5:25
[25]Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 


6:KWA KUSHAURIANA NA KUONYANA KUHESHIMIANA(1Wathesalonike.5:12-22)


Ndoa huhitaji kushauriana kabla hujafanya kitu sharing na mwezako Pia Kama Amekosea muonye kwa Kukaa naye nakumuelekeza kwa sauti nzuri usimfokee au Kumgomba mwezako pia mheshimiane nyinyi  kwa nyinyi ndani ya ndoa Yenu.


TUSOME ANDIKO;

1 Wathesalonike 5:14
[14]Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. 



         TUFANYE NINI SASA;

Tunatakiwa kuzitengeneza ndoa zetu sasa katika vile biblia inavyotuangiza kama tulivyojifunza 

Ulikuwa Pamoja nami Pastor Richard katika kukuandalia Nakala hii kwa usaindizi wa Roho Mtakatifu 


.Share Somo hili au Lisave hata kama hujaolewa litakusaindia ukija Kuolewa.