Jumamosi, 14 Juni 2025

SOMO;MALAIKA MKUU RANGUEL

SOMO:MALAIKA MKUU RAGUELI.

Karibuni Tena Mwendelezo Wa Somo letu hili la MALAIKA SABA WASIMAMAO MBELE ZA MUNGU. Ufunuo;8;2-4.

Admin; Bishop Richard Tz
Group la Maombi na Mafundisho
WhatsApp +255710889892
Join ujipatie masomo mbalimbali 

Tumetoka kujifunza Malaika wanne  
URIELI MALAIKA WA WOKOVU NA UJUZI

 RAPHAEL MALAIKA WA AFYA NA UPONYAJI

 METATRONI MALAIKA WA WATOTO 

NA MIKAEL MALAIKA WA ULINZI NA USALAMA(Hushughulika na Vita vita)

LEO TUNAENDELEA......
Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 
Ninakuletea Somo hili  litakusaindia kujua namna ya kuwatumia Malaika Hawa.


LEO TUNAENDA KUMUONA MALAIKA WA TANO ASIMAMAE MBELE ZA BWANA.

MALAIKA MKUU RAGUEL Ndiyo Jina lake huyu ni Malaika Mkuu Wa MOTO.

Huyu Malaika Amefanya kazi na Musa 
Kutoka:3:3-5 Alitokea kwa umbo la kijiti

Huyu Amefanya kazi na Elia ukisoma 1wafalme 18: Alishuka akalamba Sadaka na maji

Ufunuo 20:9 Anaoneshwa hapa akishuka kuwateketeza waovu.

Huyu alifanya kazi na Sulemani Ndani ya hekalu la Sulemani Rejea 2Nyakati;7:1

Ndiye huyu alimtenganisha Eliya na Elisha alionekana kama Gari la Moto Rejea 2WAFALME:2:10-13

KAZI ZAKE HUYU MALAIKA RAGUEL.

1;Husimamia na Kuteketeza Waovu kwa Moto.

2;Humdhihirisha Mungu kwa umbo la Moto mfano shadrack na Abnego kwenye Tanuru huyu Malaika alikuwa nao.

3;Hutokea Kwa umbo la Moto kwa muonekano mbalimbali kuligana na Vita ilivyo.

4:Husimamia watu wanaotupwa kwenye ziwa la Moto huyu Malaika huwachukua kuwatupa kule kila hukumu ikisomwa.

5:Huagamiza Miungu Huharibu Madhabahu za Shetani kwa Kuzichoma moto.

6:Yeye ni Malaika Anayeshambulia na kutetea watoto wa Mungu walio katika kipindi cha kuteswa na falme za ngiza.


NAMNA YA KUMTUMIA MALAIKA MKUU RAGUEL.

1:Naangiza Malaika Mkuu Raguel Ashuke Ashuke Akaharibu Kila madhabahu za nyumbani kwetu Ashuke na Moto wake Akaunguze Akachome Akachome katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×4


2;Moto Moto Ushuke Kutoka Mbiguni Uwateketeze Kila watesi wangu kila wanaozuia maisha yangu yasibadilike Moto moto wa Malaika Mkuu Raguel ashushe Ashushe Uokoe katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia× 4


3:Nilipo hapa hapa Nataka Leo Nimuone Raguel Malaika Mkuu Wa Moto Anashusha Moto Anaharibu Ufalme wa shetani na Wachawi wote wa mtaa huu Raguel Shuka Uwapinge Uwapinge Kwa Moto moto moto katka Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×5

4:Majeshi ya kikosi cha Moto wakiongozwa na Malaika mkuu Raguel Washuke waje wazunguke zunguke kwenye nyumba yangu katika Jina la Yesu.Amen 

Rudia ×7


HITIMISHO 

Tunapaswa kuwajua Malaika na Tuwatumie katika Vita vyetu waje watusaindie Tumia Malaika.

Nikuombe Share masomo haya yaliyokuja na nguvu ya kufungua watu kupitia Malaika wakuu wasimamao mbele za Bwana.


Naitwa Pastor Richard Wa Morogoro 
Kutoka Kanisa la Holy Spirit church Tanzania 
Makao Makuu Morogoro 


Jumamosi, 7 Juni 2025

MALAIKA MKUU MIKAELI

    SOMO; MALAIKA MKUU MIKAELI.


KIUMBE wa roho anayeitwa Mikaeli hatajwi mara nyingi katika Biblia. Hata hivyo, kila mara anatajwa akitenda jambo fulani. Katika kitabu cha Danieli, Mikaeli anapigana na malaika waovu; katika barua ya Yuda, anabishana na Shetani; na katika Ufunuo, anapigana na Ibilisi na malaika wake waovu. Anapoutetea utawala wa Yehova na kupigana na adui za Mungu, Mikaeli anatenda kupatana na maana ya jina lake—“Ni Nani Aliye Kama Mungu?” Lakini Mikaeli ni nani?

Nyakati nyingine, watu huitwa majina mbalimbali. Kwa mfano, mzee wa ukoo Yakobo aliitwa pia Israeli, na mtume Petro aliitwa Simoni. (Mwanzo 49:1, 2; Mathayo 10:2) Vivyo hivyo, Biblia inaonyesha kwamba Mikaeli ni jina lingine la Yesu Kristo, kabla na baada ya maisha yake duniani. Hebu tuone sababu za Kimaandiko zinazotufanya tukate kauli hiyo.

Malaika Mkuu. Neno la Mungu linamwita Mikaeli “yule malaika mkuu.” (Yuda 9) Ona kwamba Mikaeli anaitwa yule malaika mkuu. Hilo linaonyesha kwamba kuna malaika mmoja tu aliye mkuu. Isitoshe katika Biblia, jina “malaika mkuu” linatumiwa katika hali ya umoja tu, wala si kwa wingi. Zaidi ya hayo, Yesu anahusianishwa na wadhifa wa malaika mkuu. Kuhusu Bwana Yesu Kristo aliyefufuliwa, andiko la 1 Wathesalonike 4:16 linasema: “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni akiwa na mwito wenye amri, kwa sauti ya malaika mkuu.” Kwa hiyo sauti ya Yesu inafafanuliwa kuwa sauti ya malaika mkuu. Basi, andiko hilo linadokeza kwamba Yesu mwenyewe ndiye Mikaeli yule malaika mkuu.

Kiongozi wa Jeshi. Biblia inasema kwamba ‘Mikaeli na malaika zake walipigana na yule joka mkubwa na malaika zake.’ (Ufunuo 12:7) Kwa hiyo, Mikaeli ni Kiongozi wa jeshi la malaika waaminifu. Pia kitabu cha Ufunuo kinamtaja Yesu akiwa Kiongozi wa jeshi la malaika waaminifu. (Ufunuo 19:14-16) Naye mtume Paulo anamtaja kihususa “Bwana Yesu” na “malaika zake wenye nguvu.” (2 Wathesalonike 1:7) Kwa hiyo, Biblia inataja Mikaeli na “malaika zake” na Yesu na “malaika zake.” (Mathayo 13:41; 16:27; 24:31; 1 Petro 3:22) Kwa kuwa Neno la Mungu halionyeshi popote kwamba kuna majeshi mawili ya malaika waaminifu mbinguni—moja likiongozwa na Mikaeli na lingine likiongozwa na Yesu—ni wazi kwamba Mikaeli si mwingine ila ni Yesu Kristo akiwa katika wadhifa wake mbinguni. *

MASWALI NA MAJIBU YA BIBLIA

Shetani Alitoka Wapi..?

Swali: Je shetani yule audanganyaye ulimwengu alitoka wapi?


Jibu: shetani kwa asili aliumbwa na Mungu, na kabla ya kuwa shetani alikuwa akiitwa “Kerubi afunikaye”

Ezekieli 28:14 ” Wewe ulikuwa KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA AFUNIKAYE; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto”.

Na MUNGU alimwumba akiwa mkamilifu (asiye na dosari) kama tu MAKERUBI wengine, lakini baadaye moyo wake uliinuka akajidanganya mwenyewe kuwa anaweza kuwa kama MUNGU (aabudiwe kama MUNGU) Na ndipo Uovu huo ukaonekana ndani yake, na hakutaka kubadilika.

Ezekieli 28:15 “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”

Na baadaye alipoasi ndipo akawa shetani, na maana ya shetani ni Mshitaki/Mchongezi, maana yake anawashitaki wanadamu mbele za MUNGU mchana na usiku.

Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10  Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU”.



Swali la 2


SWALI LA PILI

. Tukio la Yesu kupaa kwenda mbinguni lilitukia eneo gani?. N.b weka andiko ku sapoti jibu lako


JIBU:    Mlima wa mzeituni. Matendo ya Mitume 1:12 [12]Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato.


Mlima wa mizeituni..ambayo inapatika kati eneo la Bethania


Luka 24:50-51 [50]Akawaongoza *mpaka Bethania*, akainua mikono yake akawabariki. [51]Ikawa katika kuwabariki, *alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni*



Swali la 3

Swali: Tunasoma Simeoni alipomwona mtoto YESU, Alikiri kuuona Wokovu wa MUNGU, sasa swali ni Wokovu gani huo alioupata?


Jibu: Tuanzie ule mstari wa 25 ili tuweze kuelewa vyema…

Luka 2:25 “Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26  Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27  Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28  yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29  Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30  KWA KUWA MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU WAKO,

31  Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

32  Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli”

Sasa hapo hajasema AMEUPATA WOKOVU..La! bali anasema “MACHO YANGU YAMEUONA WOKOVU”.. kuuona wokovu na kuupata wokovu ni vitu viwili tofauti…

Wokovu wa Mungu unapatikana kupitia mmoja tu, naye ni YESU KRISTO (Matendo 4:12),..Baada ya YESU kusulibiwa ndipo watu wakaanza kuupata wokovu, lakini kabla ya hapo waliusikia na kuuona tu,…waliousikia ni manabii wa kale na watu wote wa agano la kale, na waliouona ni watu waliokuwepo kipindi BWANA YESU anazaliwa, na walioupata ni wote waliomwamini baada ya kufufuka kw

Je Kuna Haja gani Ya Kuamini Biblia Iliyoandikwa Na Watu?

Je kuna haja gani ya kuamini biblia iliyoandikwa na watu?

Swali: Biblia imeandikwa na watu, (kama Paulo, Petro, Musa, Daudi na wengineo) je tutaamini vipi kitu kilichoandikwa na wanadamu kuwa ni kweli,? vipi kama wametoa tu kwenye akili zao, kwanini tukiamini kitabu cha namna hiyo, chenye mikono ya wanadamu?

Jibu: Kabla ya kujibu swali hili, tusome kwanza maandiko yafuatayo…

Yohana 14:11 “Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, SADIKINI KWA SABABU YA KAZI ZENYEWE”

Hapa Bwana YESU anatoa njia za sisi kumwamini yeye, kwamba kama hatutamwamini kwa yeye kutuambia kwa mdomo wake mwenyewe, basi tumwamini kupitia zile kazi anazozifanya ambazo ni ishara na miujiza.

Hiyo hakika ni hekima kuu sana!… kwamba kama sisi ni kazi sana kumwamini yeye kwa maneno ya kinywa chake, basi tuzipime zile kazi anazozifanya ikiwa ni halisi na za kweli, basi tumwamini kwahizo pasipo hata maneno yake.

Vile vile na hata kuhusiana na waandishi wa Biblia, kama hatuwaamini kuwa wameandika mambo waliyovuviwa na MUNGU, basi kupitia matokeo ya kazi hizo, (jinsi yanavyobadilisha watu wengi leo, na kuponya watu wengi) basi tuamin