Rejea Yona:1 Sura yote. Yeremia:1 Sura yote. Kutoka:3 Sura yote. Isaya. 6 Sura yote.
Watu wengi Leo Wanapitia Matatizo kwa Sababu Waliitwa wakafanye kazi ya MUNGU wakaenda kufanya vitu vingine Sasha kila wafanyacho hakiendi Audi Ameruhusiwa awatese nakuwashinda Sababu Wamekimbia Wito.
Naitwa Askofu Richard Julius Kushoka Nipo Morogoro Makao Makuu ya Makanisa Ya Holy Spirit Church Tanzania.
1:Kuwa na Visingizio Visivyoisha Kwenye Wito wake. Yaani Unapopewa ratiba ya kufanya huduma kanisani una Sababu kibao kila siku Udhuru.
2:Kufatwa na Watu wengi Wanakuambia Neno lile like La Wito wa Kumtumikia MUNGU.
3:Kuota Ndoto Unahubiri au upo kanisani Ndoto za kanisani Kanisani tu mara unaombea watu unawafungua watu unawaombea.
4:Kila Kitu Kinaanza Kufa Chochote Unachofanya Kinakufa yaani unaanza kupitia majanga Yasiyoisha Yaani unajikuta unateseka KWELI KWELI.
5:Malengo Yako Yanakufa Unakuwa upo unaishi bila malengo Heshima inaondolewa Unakuwa unadharaulika na kuchekwa.
6:Adui Zako Wanaanza Kukushambulia na Watakushida Yaani zitaimbuka kesi ambazo hukutengemea zitakurudisha nyuma Sana.
7:Unaanza Kukosa Amani Moyoni Sauti inakuwa inajirudia Nitumikie Nitumikie Mimi.
8:Watu Wanaanza Kukuita Mchungaji MTUMISHI wa MUNGU Wanakuomba unaombea na ukiwaombea Mambo Yao yanaenda vizuri
9:Unaanza Kubadilika Tabia Za Kimwili unaanza Kuchukia dhambi unaanza kutamani watu waache dhambi Wamrudie MUNGU.
10:Unaanza Kujiona Unanguvu Fulani ya kuwasaindia watu lakini hujui unaitumiaje.
HIZI NI ISHARA KUU 10 ZINAZOKUJULISHA UMEITWA NA UKIENDELEA KUWA NA SHINGO GUMU Utajikuta kila utakapoenda kukaa unasababisha Matatizo nyumba Kukosa Amani Utajikuta hupendwi Na kila MTU kila atakayekusaindia Maisha yake au ndoa yake itaharibika.
Unaweza Ukawa Unasababisha Matatizo Kwenye kampuni au Kazi Za Watu Kisa Umekataa Wito MUNGU Anakuadhibu.
TUNAFANYA NINI KAMA HIZI DALILI NINAZO.
Kwanza Hongera Ukijigudua Hizi Dalili unazo Sauti itaanza kujirudia Kusema na Wewe Juu Ya Somo Hili.
. Fanya Haya .
Kanisa LA Holy Spirit Church Tanzania Moto Wa Yesu Tunachuo Cha Thiolonjia Tumejitoa Kuinua Vijana Wa Kike na Wakiume Wenye Wito Wa Kwenda Kumtumikia Mungu.
Utatakiwa Ufike chuoni ujaze fomu na uanze masomo ya uchungaji na ukimaliza ni Jukumu letu kukupeleka mkoa ulioitiwa Ukafanyie Kazi Ya Mungu Utatumika china Ya Holy Spirit Church Tanzania lakini ukisema unakuja kusoma tu unadhehebu lako litakalokubemba haina shida.
UTARATIBU WA CHUONI HAPA.
Ukija hapa Nidhamu na Heshima na utii ndivyo vitakavyokufanya ufunzu Uchungaji.
Kula Utajigharamia. Kulala Hosteli Bureee Maji Bureee Umeme Bureee Masomo Bureee English Course Bureee Cheti Bureee Kwa Wanaotumika Na Kanisa Hili nje ya Kanisa Hili Chet Utachangia 50000 tu.
MUDA WA KUKAA DARASANI.
Kuna ngazi mbili za Masomo
. Wanaokuja kusomea Chet.
Miezi sita watakaa chuoni
Wanao Somea Diploma
Ni Mwaka Mmoja Ukiwa chuoni na umetulia na Kwa Wanao taka KUWA Wachungaji Wa Holy Spirit Church Tanzania Tuna chukua wanaokuja kukaa Mwaka Mmoja ili kuwasoma na kuwajua vizuri nao kupata elimu kubwa juu ya Utumishi wao.
JINSI YA KUFIKA CHUONI KWETU.
Chuo hiki Kipo Morogoro Dakawa High School nyuma ya hii shule ya waschana Dakika 45 Kutoka Morogoro mjini.
Panda Gari Zinazokuja Morogoro Ukishuka Msamvu Sted chukua Gari Za Kuja Dumila 4000 Waambie Nashukia Veta Dakawa Chukua Pikipiki Waambie naenda Moto Wa Yesu au Kwa Pastor Richard.
Ukija chuoni hurusiwi Kutoka bila ruhusa ya uongozi Wa chuo.
MAWASILIANO.
.Mwenyekiti Bishop Richard 0759861768
Katibu:Pastor Felix:0659498191
Ukiwa Unakuja Tumia hizo Namba Katibu Tukutengeneze UKAWE Pastor aliye Moto moto ukaokoe roho za watu.
WhatsApp inbox +255710889892 Tunapokea watu nchi zote imladi Uwe na Wito na utayari Wa kutumika.