SOMO: MAOMBI YA UKOMBOZI WAKUJITOA KWENYE MIKATABA YA KIKABILA
Vitabu Rejea;Kutoka:31:1-11, HESABU;7;30-40, ZABURI:78;67-72 WARUMI;11;1-10,
WAEBRANIA;7;11-28
Karibu
Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Kanisa la Holy Spirit church Tanzania
KABILA NI NINI..?
Kabila Ni Umoja Wa Jamii Fulani Yenye Desturi na Utamaduni Mmoja Lugha moja Wanokuwa wapo ndani ya Taifa fulani au nchi moja..?
Mfano Tanzania Kuna Kabila la Wasukuma,Wachanga.Wangoni,Wanyakyusa nk Jumla kuna Kabila 120
Hizi Kabila Kila Kabila inatamanduni yake na Lugha yake ya utambulisho wa hilo Kabila.
MAOMBI YA KUJITOA KWENYE MIKATABA YA KIKABILA.
Hii ni hatua ya mtu aliyepata Neema ya juu kumjua Mungu akatambua kabila lake kuna vitu linafanya inakuwa chukizo kwa Mungu inamfanya Mungu alitese kabila hilo naye anakuwa ni wa kabila hilo lazima Avenue hiyo mikataba ajiondoe kwenye laana hizo.
Yoshua:7:1-18
Wapo Watu Hawaolewi au Kuowa Sababu ya Sifa mbaya ya Kabila lao.
Wapo Watu Wanaolewa au Kuowa Kupitia Sifa Nzuri za Kabila Lao.
KWA UFUPI KABILA LAKO LINANGUVU YA KUKUTAWALA NA KUKUTAMBULISHA VIZURI AU VIBAYA HAIJALISHI UMEOKOKA UMESOMA HUJASOMA Kabila linanguvu.
Mfano Kabila La Wafipa Wachawi hii inamtambulisha hivyo kila mfipa.
Kabila la Wasukuma Wapenda Uganga na udikiteta hii sifa inakufunga kila Msukuma.
Mfano: Wachanga Ni Wanapenda Pesa Matambiko Ulevi Kila mchanga ukisema tu kabila lako watu wanakuja kutazama sifa.
Wakinga Wanapenda Biashara na Mali Za Madawa Ukiwa tu Mkinga hata kama umeokoka unabembwa na sifa hiyo.
Wahaya Wanapenda Majivuno Hata Kama Umeokoka ukisema tu mhaya wanajua
Wahehe Hasira na Kujinyoga Ukisema tu mimi mhehe wanajua unatabia hiyo.
Wagongo Ulevi na Kuachika kwenye ndoa na Kuomba omba
HIZI NI BAADHI YA TABIA MBALIMBALI ZA MAKABILA.
MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOOMBA
1;Lijue Kabila lako Watu wanalitambua Kwa Sifa za Tabia ngani ..?
2:Utakayeomba mlengwa mwenye kabila hilo..?
3:Utafata Hatua ninazoenda Kukuongoza.
HATUA ZA KUFUATA UNAPOOMBA.
1:OMBA KUSHUGHULIKIA KUJIONDOA KWENYE TABIA ZA KABILA LAKO.
Ninajiondoa kwenye Tabia Za Kikabila Zilizouganishwa Ndani Yangu Kuniharibia sifa yangu ya Wokovu Katika Jina la Yesu.Amen ×3
Endelea kuomba Tamka maneno unayoona yanakuja kinywani.
2:OMBA TOBA KWA AJILI YA KABILA LAKO:
Baba Yangu Nakuja Mbele Zako Nalibeba Kabila Langu Naomba Unisamehe mimi na Kabila langu limekuwa like-minded nakutembea katika Imani Inayokuudhi Katika Jina la Yesu.Amen
Endelea Kuomba Toba Kwa Ajili ya Kabila lako
3:OMBA KUVUNJA MIKATABA MBALIMBALI NA MAPOKEO YA WATU WANAOTUMIA KABILA LAKO KUZUIA BARAKA ZAKO.
Hapa utashughulikia kila utambulisho ulio mbaya wa kabila lako weka Utambulisho mzuri
Ninakataa kabila langu kuwa na utambulisho ulio mbaya utambulisho usiofaa kwenye Jamii hali inayonifanya hata mimi nikose mke wa kumuowa Nikose Mume wa Kuniowa Navunja Kila Mikataba Makubaliano yaliyowekwanga na Waazilishi wa Kabila langu Kila uhalali adui ambao aliupata kwenye kabila langu achia achia mimi ni mtoto wa Mungu Kabila wa Simba wa Yuda Katika Jina la Yesu.Amen
Endelea kuomba huku unatembeatembea Tamka Maneno Tamka huku Unaomba Kadiri Roho Mtakatifu Anavyokuongoza.
Mwanangu Mungu akupe Kunielewa Zaidi Maombi Haya Yanaitaji Uelewe Kuna nguvu inayowafanya Watu Wasiolewe au Kuowa iliyo ndani ya Kabila lao.
Kuna nguvu kubwa kwenye Kabila lako.